Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 17 pande za nchini China ameiuza figo yake ili aweze kununua simu aina ya iPhone na iPad.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na magazeti ya China, kijana huyo anayeitwa Xiao Zheng alifanyiwa operesheni na kuitoa figo lake moja kwenye jimbo la Hunan mwezi aprili mwaka huu.
Pesa alizolipwa kwa kuuza figo lake kijana huyo alinunua simu ya i
Phone na kompyuta ndogo ya iPad.
Xiao aliuza figo lake kwa yuan 20,000 ambazo ni sawa na Tsh. milioni 4.5za kibofongo hivi.
"Wakati mtoto wangu aliporudi nyumbani akiwa na kompyuta ya iPad na simu ya iPhone, nilimuuliza amepata wapi pesa za kununulia vitu hivyo, haukupita muda mrefu alitoboa siri kuwa ameliuza figo lake moja, nilihisi kama dunia inatuangukia", alisema mama yake huyo dogo.
Mama yake Xiao aliripoti polisi lakini hadi sasa hawajafanikiwa kumkamata mfanyabiashara aliyenunua figo yake.