Saturday, August 13, 2011

TANZANIA YAPINGA MCHEZO WA BIG BROTHER!!!!!!!!!MMMMMMM!!!!!!

SERIKALI imepinga Tanzania kushiriki shindano la Big Brother Afrika kwa kuwa shindano hilo linapotosha maadili ya kiafrika na kuharibu kizazi cha watoto wa Tanzania.

Akizungumza bungeni , Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Emmanuel Nchimbi amesema shindano hilo ni kero kubwa kwa serikali na taifa kwa ujumla na hawajui linafundisha nini kwa jamii.

"Hatujui linafundisha nini watoto wetu, linapotosha jamii, ni kero kubwa hatushabikii shindano hili na wanaoenda kushiriki wajue hawana baraka za serikali ndio maana hatujawahi kwenda k


uwapokea na bahati yao mawasiliano yao ya kushiriki wanafanya kwa njia ya mtandao,"alisema Nchimbi.

Alisema shindano hilo limekuwa likichochea uvunjifu wa maadili kwa washiriki na hata kwa wale wanaobaki nchini.

Kauli ya Nchimbi imekuja baada ya wabunge kuhoji umuhimu wa shindano hilo ambalo limekuwa likichochea vitendo vya ngono kutokana na kuonyeshwa live kila kitu kinachoendelea ndani ya jumba hilo kinyume na maadili ya kiafrika.

Hivi karibuni mshiriki wa Tanzania, Bhoke Egina alikumbwa na kashfa kubwa ya kujiingiza kwenye uhusiano wa mapenzi na mshiriki toka Uganda Enerst.

Washiriki wengine watanzania walioshiriki shindano hilo na hawakukwepa kashfa ya kujiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi ni Mwisho Mwampamba, Richard Benezueout na Latoya.

Shindano hilo huandaliwa na M - Net Afrika na kurushwa moja kwa moja na kituo hicho, limekuwa likifanyika nchini Afrika Kusini kwa kushirikisha nchi zaidi ya 20 barani Afrika.