Wednesday, May 18, 2011

SHCWARZENEGGER NA SKENDO CHAFU INAYOMKABILI........!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mkongwe wa filamu maarufu duniani na gavana wa zamani wa jimbo la California,Arnold Schwarzenegger inasemekana ameitelekeza, ambapo sababu ya kuvunjika kwa ndoa hiyo imeelezwa kuwa ni baada ya Arnold kumla uroda na kuzaa na hausigeli wake aliyekuwa anapiga kazi home kwake.

Ndoa ya Arnold Schwarzenegger ambayo ilidumu miaka 25 ya ilivunjika hivi karibuni na kitendo cha Arnold Schwarzenegger kuwa na u


husiano wa kimapenzi na hausigeli wake inasemekana ndio chanzo cha kuvunjika kwa ndoa hiyo na Schwarzenegger alimuomba msamaha mkewe wake, Maria Shriver na familia yake akisema kuwa sababu ya kuvunjika kwa ndoa yao ni mtoto wa nje ya ndoa ambaye alizaa na hausigeli huyo miaka 10 iliyopita.
Hausigeli anaitwa Mildred Patricia Baena na kwa miaka 20 alikuwa akifanya kazi za ndani nyumbani kwa na alikuwa akipokea mshahara mzuri wa dola 1,200 kwa wiki, ambapo Patricia kwa sasa ana miaka 50 na ameshastaafu kazi na aliwahi kuwaambia marafiki zake kuwa alikuwa akifanya mapenzi na Arnold bila ya kutumia kinga ndani ya nyumba ya Arnold na Alipopata ujauzito hakumwambia Arnold ambaye baadae alikuja kugundua baada ya mtoto huyo wa kiume kuzaliwa na kufuatia kugundulika kwa siri hizo za ndani, mke wa Arnold,Maria Shriver mwenye umri wa miaka 55, ametangaza kuwa atatoboa siri zote atakapoenda kwenye shoo ya Oprah Winfrey baadae mwaka huu kuhusiana na taarifa hiyo.