Tuesday, April 10, 2012

HII NI MAKALA ALIYOANDIKA MTANGAZAJI WA GENERATION FM KUHUSIANA NA JK KUTOA MIL.10 KTK MSIBA WA KANUMBA!

Yassin Wakwanza Juma
about an hour ago · .NAJUA WENGI WATACHUKULIA KIVINGINE LAKINI HUU KWA UPANDE WANGU NI UKWELI KABISA TENA UNAOUMIZA SANA..........
BORA NISEME NIWE NA AMANI

Makala haya, labda nayaandika huku tukiwa katika huzuni kubwa lakini kilichotokea hakiwezi kubadilishwa tena. Wengi watamzungumzia walivyomfahamu marehemu kwa kadri wanavyoweza, asilimia kubwa wakimsema kwa mazuri aidha kinafiki ama kutoka moyoni, wapo wanaolia kutokana na huzuni huku wengine wakiwa katika maigizo ya kawaida ya kutoa machozi. Hata wanafiki wapo wanajigalagaza na kujidai wanazimia ili waandishi waje kuwapiga picha. Na wengine wanazimia kutokana na mbanano lakini media zetu zitaandika mengine.
Asanteni wote ambao msiba umewagusa kwa namna ya kipekee. Na tujipe pole wale wote tuliojipeleka kimbelembele mapema pale Leaders club kama walivyotusisitiza kwenda kuaga halafu tukatemwa na kusahaulika umuhimu wetu kama mate yakishatoka mdomoni. Wameaga wanaojidai wana uchungu zaidi kuliko wote!!!! Hata kumwona mara ya mwisho tumeshindwa, nawachukia sana hawa jamaa waliojidai wao ndio waol na kuzima maamuzi ya familia

Ishu yangu leo ni kama ipo kisiasa lakini mimi hizo siasa sina huwa naweka wazi hisia zangu na mwisho wa siku natambua ujumbe unafika hata kama unamuumiza mtu!!!

Mkubwa wa nchi hii alikuwa mmoja kati ya watu wakubwa na kuheshimika kufika nyumbani kwa marehemu, jambo moja ambalo nililifurahia mwanzoni lakini leo hii nagundua sio jema ni kitendo cha jamaa kutoa shilingi milioni kumi kama rambirambi pale msibani kiukweli nimefikiria mengi sana, kwanza ni huu msiba, najua wajua kuwa huu sio msiba wa kitaifa japo umeligusa taifa. Sio kwamba nafurahia roho hii kutoweka, hapana marehemu alikuwa muhimu sana japo roho yake na ya babu yangu kijijini zote ni za kutoka na kurudi kule kule. “ROHO ZOTE NI SAWA USONI PA MUNGU!! ILA ZINATOFAUTISHWA NA UCHA MUNGU!! PEKEE”

Mkuu wa nchi ameonyesha udhaifu wa hali ya juu sana. Milioni kumi haikuwa pesa ndogo kama unavyoweza kuichukulia hasahasa katika kipindi hichi kigumu. Mkuu wetu wa nchi anaonekana bado ana ‘ujana’ ndani yake bado anatafuta kitu kinachoitwa sifa bila kutazama maslahi ya taifa letu.

Madaktari waligoma hapo majuzi, baba mama dada na kaka zangu walipoteza uhai kwa uzembe huu wa kushindwa kuwatimizia madaktari kile walichokuwa wamekitaka na baada ya vifo hivyo eti wakaongezewa malipio, sasa sijui serikali iliweka rehani roho za wapiga kura wake???
Halafu ulipanda ndege ukawa kama umeikimbia nchi, ukituacha katika vilio. Lakini nasikia hii ishu imesababisha ughaili safari ya kwenda huko sijui wapi kikazi. Yaani Baba wewe kwa kweli mi nasema baaaado!!!!

Ameugua mzee Kipara, nguli wa sanaa za maigizo hapa bongo, hakuna hata michango ya maana iliyoenda kuokoa roho yam zee huyu, akafariki!!!! Sikumbuki kama ulienda ama uliagiza mtu!!!!
Haya leo umetoa milioni kumi katika msiba ambao michango ya watu kadhaa ilikuwa inaweza kumzika katika kiwango hichi hichi alichozikwa JE AKIFA MSANII MWINGINE TENA UTATOA MILIONI KUMI AMA?? Siombei mabaya lakini jiulize itajengeka picha gani???. Baba siamini kama ulifikiria juu ya watoto wanaokaa chini huko kijijini kwetu, dawa za wagonjwa wa kifua kikuu zinaisha baba wanakufa tu mahospitalini na wengine majumbani huku.

Yaani binafsi ningekuona umefanya jambo la maana sana kama ungekuwa umewasaidia wasanii kabla hawajarejea mavumbini. Mtazame huyu bwana anayejiita STEPS……Hivi unajua kwamba marehemu na wasanii wengine hawachangii kabisa pato la taifa kwa sababu ya mambo ya kijanja janja yanayoendelea….anafaidika huyu STEPS. Sio mtanzania huyo baba, mimi sio mbaguzi wa rangi lakini haki za wasanii wetu ziko wapi sasa. Tazama hawana urithi wowote ule wafiwa, mtanzania usijidanganye na kazi nyingi za marehemu ukadhani ndo waliosalia wamepata utajiri, HAKUNA kazi zote zile alizofanya sio za kwake kashaiuza haki yake, kwa hawa WAHINDI!!!! Baba unaliona hili wewe, ama ndo vile kwa kuwa ni tukio la watu wengi tuone jinsi unavyowajali wasanii???? Huo ni unafiki baba!!!!!!

Watazame sasa wasanii, kama wakiwezeshwa hizo pesa ulizomwaga bila kujifikiria utawapatia waalimu kutoka vyuoni ambao serikali iliwapatia kilo saba za mchele na maharage kilo tatu eti wazitumie kwa mwezi mmoja. Baba kamati zako zina akili timamu na upendo kweli ama wanapuuzia watu wa hali ya chini na kujionyesha kwa wenye pesa??? Ndio hivyo unadhani tutafikiriaje sisi huku kijijini, babu na bibi kijijini wakisikia umefanya mambo kama haya unadhani watakuelewa baba….hebu sema mwenyewe MILIONI KUMI YA NINI?????? KWA NINI WASITOE PESA HAO STEPS WANAOTUIBIA KILA SIKU, Tena walitakiwa watoe kwa AMRI BABA!!!!! Yaani kama ungefanya hivyo ningekuona wa maana sana katika harakati za ukombozi!!!! Haiwezekani hata kidogo hawa jamaa wanachukua haki zetu kirahisi hivi, halafu tunabaki kugombana sisi kwa sisi Bongo Movies na TAFF!!!!!! Si umewasikia msibani sijui huyo muhindi anazungumzia HASARA atakayoipata baada ya Kanumba kuwa amefariki, huyu jamaa ni shetani MKUBWA aisee yaani unahojiwa unazungumzia hasara badala ya kuitazama ROHO!!!!!!!

Wao wanakula pesa wanaondoka. Haiwezekani eti mtu anatunga filamu anapewa milioni 20, naye anaridhika wakati hiyo milioni 20 ni sawa na watu 5000 kununua kazi hiyo, haya sasa watanzania tupo wangapi, tazama wajanja hawa wanavyotugandamiza baba!!! Tumekulilia mara ngapi wewe, mbona haujatujali, sasa hiyo pesa uliyotoa unadhani imeyaziba yale uliyojisahaulisha???? Pesa yako hiyo haijanufaisha chochote zaidi ya wajanja kadhaa waliokodolea macho pesa za rambirambi!!!!

Kwenye msiba wa mzee Kipara sijui walitoa laki ngapi vile,hawa jamaa eti kisa hajahusika katika filamu zao za STEPS kwa sana. Hawa sio wazuri baba??? Angalia nawewe unajichafulia jina lako zaidi aaah!!!!!

Sijamalizana na wewe baba, lakini kuna huu upande wa pili, hawa jamaa wa CHADEMA HAWA. Hivi hamjawahi kusikia kesi nyingine ama huyu LULU ndo kesi ya kwanza inayohusika na mauaji???? Mbona mwaleta siasa katika mambo yanayotuumiza kama haya. Kesi ya yule mtoto RAMA aliyekutwa na kichwa cha mtu mbona hamkusikika au kuna nini hapa kwa LULU??? RAMA yupo segerea sasa hivi mshawahi kuzungumzia hata hatma yake?? Sasa naduwaa eti mara Halima Mdee ameenda na cheti cha kuzaliwa mara sijui nini mbona RAMA alikuwa na miaka 16 wakati ule??? Binafsi nimekereka sana, halafu na huyu mama yake na Lulu, mbona wakati haka katoto kanafanya bethidei na kusema kametimiza miaka 18, mama alikaa kimya?? Halafu leo hii ananyanyua kinywa chake eti ‘mwanangu ana miaka 17” mimi simuhukumu lakini hizi siasa na zikome na sheria ichukue mkondo wake sasa!!!!! Kama she is innocent na iwe hivyo kama ni vinginevyo na hatua zichukuliwe.

Yaani siasa hizi zinakera na zinaonyesha ni jinsi gani tunakuwa na ubaguzi kwa walionacho na wasionacho. Mmeshindwa kuwatetea akina Babu seya na wanawe ambao hawajatoa roho za watu eti leo ghafla bin vuu LULU. Kwani yeye ni nani?????? Msitufanye sisi wajinga aiseee!!!! Mimi nasema haya najua wapo ambao hawawezi kusema, japo wanaumia mno!!!.

Waalimu wanalia kila siku maisha magumu, shule zina upungufu wa vifaa, miundombinu mibovu, maisha kwa ujumla yanapanda, nauli za daladala, bei za mchele na sukari. Halafu kweli baba unaenda kutoa milioni kumi wakati ulisema serikali haina pesa wakati unagoma kuwaongeza madaktari pesa hadi ndugu zetu wakafa hadi mochwari zikajaa maiti zikawa zinawekwa chini….ni nini kikuu katika hili mzee wetu??? Sikumsikia Obama kutoa mamilioni Michael Jacks alipotoweka, najua alituma mwakilishi kwenda kwenye mazishi lakini wewe baba unafanya mambo kama anayofanya mwernyekiti wa klabu ya Simba yaani yeye kila kitu, msemaji wa klabu yupo lakini kila jambo yeye hadi sasa amezoeleka. Mbona nawe unatufanya tukuzoee upesi hivyo.

Haya basi hata kama umetoa hiyo pesa ungefanya kimya kimya basi tusijue huku kijijini ambapo hospitali hazina madawa, ungefanya kwa siri baba wasisikie waalimu wanaoteseka kila siku, ungefanya kwa siri ili wale wazee wa TRL wasisikie maana uliwatesa sana, ungefanya kwa siri na watoto wa mitaani nao wasikusikie maana vilio vyao ni LAANA, ungefanya kwa siri basi zisikusikie zile nchi zinazotupa msaada maana Watadhani sisi matajiri baba, hivi kwa mfano wakikuuliza kwa nini umetoa milioni kumi utajibu nini???. Mkuu wangu sikutukani lakini ulichofanya UMEKURUPUKA na KUTAFUTA sifa zisizokuwa na maana.
MIMI NIMEMALIZA KINYONGO CHANGU!!!!! MOYONI SAAAAFI!!!!
LikeUnlike · ·Unfollow postFollow post · Share.
Elifazi Doctorfazi Mtwale and Grace Sambwe like this..

COMMENTS......

1.Hamis Mhando Daah! br. umenena, ila nnachokuomba makala hii iwekwe gazetin coz ktk fb inawafikia wachache wenye uwezo wa kutumia fb hao wengine watajuaje machungu haya?
Lingine, we unafikir baba alikusudia nin kutoa kiasi hicho jaji ktk mtazamo chanya ili sisi wazito kuelewa tupate kutafakar kwa pande zote kisha tufanye maamuz sahihi.15 minutes ago ·